LONDON, Uingereza
KLABU ya Chelsea imetangaza usajili wa kiungo kutoka Wigan Athletic, Harrison Bettoni, ambaye amesaini mkataba wa miaka minne.
Bettoni (18), alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Wigan msimu wa 2025-26, ambapo alicheza mechi 27.
Katika mechi hizo, nyota huyo alifunga mabao manne, likiwamo alilofunga katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya AFC Wimbledon.
Kama itakumbukwa, alicheza pia mechi ya raundi ya nne ya msimu huo wa michuano ya FA dhidi ya Washika Bunduki wa London, Arsenal.
Nyota huyo amekuwa na Wigan tangu aliposajiliwa kwenye ‘academy’ ya vijana wenye umri chini ya miaka 13 mwaka 2019.


