24.9 C
New York

WAFCON 2026: Nini hatima ya makocha wanawake?

Published:

CAIRO, Misri

FAINALI za mwaka huu Mataifa Afrika kwa timu za soka za Taifa za Wanawake (WAFCON 2026) zitaanza kutimua vumbi Julai 26, 2026.

Timu 16 zitatoana jasho, huku nne tu zikiongozwa na makocha wanawake kwenye mabenchi ya ufundi. Timu hizo ni Cameroon, Zambia, Kenya, na Afrika Kusini.

Zilizobaki ziko chini ya makocha WA kiume, zikiwa na wasaidizi wanawake kama ilivyoelekezwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Kwa makocha wakuu wa kike wanne, sawa na asilimia 25, fainali za mwaka huu ni tofauti na zilizopita (2025) zilizokuwa na wawili pekee (16.7%).

Afrika Kusini inaye Desiree Ellis ambaye aliipa timu hiyo taji la WAFCON mwaka 2022. Ametwaa mara nne tuzo ya Kocha Bora wa CAF kwa upande wa soka la wanawake.

“Shirikisho letu limepiga hatua kubwa ya kutaka timu zote za wanawake ziwe na makocha wa kike,” anasema.

Hata hivyo, Ellis anasisitiza kuwa kumteua makocha wa kike pekee haitoshi, bali pia wapewe sapoti ili kufikia mafanikio.

Related articles

Recent articles