24.9 C
New York

Nini kiliwakutanisha Trump, Rais wa Lebanon?

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Lebanon, Joseph Aoun, alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake nchini Marekani, Donald Trump, mapema wiki hii.

Ziara ya Rais Aoun ilikuja wakati huu Lebanon ikiishinikiza Israel kuondosha vikosi vyake vya kijeshi Kusini mwa nchi hiyo.

Pia, ni ziara ilikuja katikati ya vita kati ya Israel na wapiganaji wa Hezbollah, kundi la kigaidi lililoko nchini Lebanon.

Wakati huo huo, Serikali ya Lebanon haikubaliani na uwepo wa Hezbollah na inapambana kulitokomeza Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran.

Hivyo, moja ya ajenda za Rais Aoun katika ziara yake nchini Marekani ni kuiomba nchi hiyo iwaunge mkono katika mambo mawili hayo.

Mosi, kuhakikisha vikosi vya jeshi la Israel vinaondoka Lebanon. Pili, kuibana na kuisambaratisha Hezbollah.

Kwa upande mwingine, ziara yake nchini Marekani imeonywa na Hezbollah, ambapo kundi hilo limesema Rais Aoun anaitafutia matatizo Lebanon.

Hezbollah hawakubaliani na kitendo cha kukaa mezani na Marekani au Israel, kwa madai kuwa nchi hizo zimekuwa zikiinyonya Lebanon, hivyo hazipaswi kupigiwa magoti.

Baada ya kuwasili Marekani wikiendi iliyopita, Rais Aoun alikutana na Katibu wa Serikali, Marco Rubio, ambaye baadaye aliahidi kuwa wataiunga mkono Lebanon kama njia ya kulitokomeza Hezbollah.

“Ndiye anayeongoza Serikali halali, ndiye tutakayeshirikiana naye na Serikali yake ndiyo inayopaswa kuongoza nchi,” alisema Rubio.

Vikosi vya Israel viko maeneo ya Kusini kwa madai ya kudhibiti mashambulizi ya Hezbollah. Kwamba Kundi hilo limekuwa hapo kimkakati, kwa kuwa ni jirani na Israel, hivyo kuishambulia kirahisi.

Katika makubaliano yaliyowahi kufikiwa awali, Israel iliweka wazi kuwa haitoondoka Kusini mwa Lebanon hadi pale itakapojirisha kuwa jeshi la nchi hiyo (LAF) limeiangamiza Hezbollah.

Hata hivyo, iko wazi kuwa Rais Aoun anapingwa na hata baadhi ya watu wake, achilia mbali Hezbollah, akitajwa kuifanya nchi yao kuendeshwa kwa amri na matamko ya Marekani na Israel.

Kwa upande wake, Rais Trump katika moja ya hotuba zake, amewahi kuitaka Israel kuondosha wanajeshi wake nchini Lebanon.

Related articles

Recent articles