9 C
New York

Salah aendeleza ubabe England

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

MOHAMED Salah amekuwa mchezaji pekee wa England aliyefunga na kutoa ‘asisti’ mara nyingi katika mchezo mmoja, kwa mujibu wa takwimu za tangu msimu uliopita.

Salah ameandika historia hiyo wakati Liverpool ilipoifunga Brighton mabao 3-0 na kutinga raundi ya tano ya Kombe la FA.

Nyota huyo wa kimataifa wa Misri alifunga na kutoa asisti na hiyo ikawa mara yake ya 15 kufanya hivyo.

Kwa takwimu zilivyo, Salah aliyewahi kupita Chelsea na AS Roma anawapiku Bukayo Saka na Erling Haaland, ambao kila mmoja amefunga na kutoa asisti mara sita.

Tangu msimu huu uanze, ameingia kambani mara saba na pasi zake za mwisho zimezalisha mengine matano.

Hata hivyo, bao alilofunga dhidi ya Brighton lilikuwa la pili kwa Salah katika mechi 13 za hivi karibuni.

Dhidi ya Brighton, Liverpool ilipata mabao mengine mawili kupitia kwa Curtis Jones na Dominik Szoboszlai.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img