9 C
New York

Simba yamlilia Ashraf

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

UONGOZI wa klabu ya soka ya Simba umeeleza kuguswa kwake na taarifa za kifo cha mwanachama wake maarufu, Is-haka Mukadam.

Mukadam, maarufu zaidi kwa jina la Ashraf, alikuwa Mwenyekiti wa Simba kwa Mkoa wa Mwanza.

Amefariki usiku wa kuamkia leo Februari 15, 2026, akiwa kwenye matibabu nchini India, ambapo alipelekwa baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu.

“Enzi za uhai wake, Ashraf atakumbukwa kwa mapenzi yake na mchango mkubwa wa hali na mali kila timu zetu zinapokuwa jijini Mwanza,” inaeleza taarifa ya Simba.

“Simba inatoa pole kwa familia, ndugu na jamaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu kwa msiba huu mzito na tunaiombea roho ya marehemu ipumzike mahala pema peponi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img