LONDON, Uingereza
LICHA ya kuhususishwa na Manchester United, Roberto De Zerbi anavutiwa zaidi na tetesi zinazomuhusisha na Tottenham.
De Zerbi, raia wa Italia mwenye umri wa miaka 46, ameshaondoka katika klabu ya Marseille ya Ligue 1.
Wakati huu Man United ikiwa chini ya kocha wa muda, Michael Carrick, inahitaji atakayeiongoza timu hiyo msimu ujao (2026-27).
Kwa upande mwingine, Tottenham haina kocha mkuu baada ya kumfuta kazi raia wa Denmark, Thomas Frank.
Ukiweka kando jina la De Zerbi, makocha wengine wanaohusishwa na kibarua cha Frank pale Spurs ni Mauricio Pochettino na Oliver Glasner.


