22 C
New York

Mataifa yenye ng’ombe wengi kuliko watu

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

HII inaweza kushangaza lakini takwimu zinathibitisha kuwa yapo mataifa ambayo idadi ya ng’ombe ni kubwa kuliko ile ya watu wake.

Kupitia mtandao wa The World in Maps, yapo mataifa manne duniani, ambayo yamethibitisha upekee wao huo.
Kwa mujibu wa The World in Maps, Argentina ni miongoni mwa hizo nchi ikiwa na ng’ombe milioni 53.8, huku watu wake wakiwa ni milioni 45.5 pekee.

Taifa hilo la Amerika ya Kusini limekuwa likitajwa kufanya vizuri katika usafirishaji wa nyama ya ng’ombe maeneo mengi duniani. Ng’ombe ni alama muhimu katika uchumi wa nchi hiyo.

Majirani zao wa Amerika ya Kusini, Brazil, nao wamo kwenye upekee huo, ambapo Taifa hilo lina ng’ombe milioni 252.7, huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 211.1.

Brazil inamikiki asilimia 25 ya ng’ombe wote wa Amerika ya Kusini na ndiyo kinara wa usafirishaji wa nyama duniani. Ufugaji wa ng’ombe ni sekta inayoheshimiwa nchini humo ikiwa chanzo cha ajira kwa mamilioni ya wananchi.

Uruguay, taifa jingine linalopatikana Kusini mwa Bara la Asia, nalo lina idadi kubwa ya ng’ombe kuliko watu. Idadi ya ng’ombe ni milioni 11.9, wakati watu ni milioni 3.3 pekee.

Nyama ya ng’ombe ya Uruguay ina soko kubwa kimataifa, hivyo kuifanya biashara hiyo kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi hiyo.

Wakati Uruguay ikisafirisha zaidi ya asilimia 70 ya nyama ya ng’ombe, soko lake kubwa ni China na mataifa ya Umoja wa Ulaya.

Kwa barani Ulaya, New Zealand inaingia pia kwenye upekee huo, ikitajwa kuwa na ng’ombe milioni 10, huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 5.2 pekee.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img