Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR
ISSA Ali Mangungu ni miongoni mwa majina yaliyochomoza katika kinyang’anyiro cha urais kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini [TPBRC].
Usahili wa kuwapata wagombea umefanyika leo Novemba 20, 2026, ambapo wengine waliopitishwa kuwania urais ni Wakili Stephen Mosha, Rwegasira Samson na Wasiwasi Mwabulambo.
Kwa upande mwingine, wagombea wa nafasi ya Makamu wa Rais waliopitishwa kupitia usahili huo ni Fredrick Lori na mwandishi mkongwe wa habari za michezo, Jacob Mbuya.
Katika nafasi ya uwakilishi wa wanawake, ni Christinah Oscar Koroso, huku Dk. Anichetus Christian Lusale akiwani uwakilishi wa Kanda ya Kati.
Aidha, Rosemary Zakaria Massawe anawania uwakilishi wa Kanda ya Kaskazini, huku ile ya Mashariki ikiwa na wagombea Bakari Khatibu, Nassoro Ally Chuma na Abdallah Juma Mtulamesu.
Wakati huo huo, mgombea kwa Kanda ya Ziwa ni Chase Donatus Masanja, wakati ile ya Magharibi ikiwa na Hashir Hamis Masangula.


