20.2 C
New York

Wanawake 600 wauawa Afrika Kusini

Published:

PRETORIA, Afrika Kusini

WANAWAKE takribani 600 wameuawa nchini Afrika Kusini kwa kipindi kifupi cha miezi mitatu ya hivi karibuni kutokana na matukio ya uhalifu.

Idadi hiyo inahuisha 13 waliouawa na miili yao kutupwa katika maeneo ya umma katika mitaa mbalimbali ya mjini Johannesburg.

Afrika Kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye kiwango kikubwa cha unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake, achilia mbali matukio ya uhalifu.

Mapema wiki hii, wanawake watano na mtoto walikatishiwa maisha kwa kupigwa risasi katika Jimbo la Free State.

Kwa takwimu zilizopo, ni wastani wa vifo vya wanawake 60 kila siku, idadi ambayo inashitua na kuviweka kwenye wakati mgumu vyombo vya ulinzi na usalama.

Related articles

Recent articles