16 C
New York

Rais Dk. Samia kuzindua kiwanda cha magari Uganda

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, atatembelea na kuzindua kiwanda cha kuunganisha magari cha Double Q Automotive Assembly Plant kilichopo Wilaya ya Mpigi nchini Uganda.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imeeleza kuwa Rais Dk. Samia anaondoka nchini leo Novemba 18, 2026, kwenda Uganda kwa ajili ya ziara ya kitaifa ya siku mbili, ukiwa ni mwaliko wa Rais Yoweri Museveni.

Aidha, akiwa Uganda, pia Rais Dk. Samia atafanya mazungumzo na mwenyeji wake huyo yatakayoangazia kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Uganda katika sekta mbalimbali.

Kwa upande mwingine, sekta zinazotarajiwa kuwa sehemu kubwa ya mazungumzo ya viongozi wawili hao ni nishati, kilimo, viwanda, biashara na fedha.

Vilevile, ziara ya Dk. Samia inalenga kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, ikiwa ni pamoja na kupanua fursa za kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Related articles

Recent articles