16 C
New York

Haaland aipeleka Norway robo fainali

Published:

LONDON, Uingereza

STRAIKA Erling Haaland ameingia kambani mara mawili na kuiwezesha timu ya soka ya Taifa ya Norway kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Denmark.

Mabao hayo, pamoja na lile la Martin Odegaard yameipa Norway tiketi ya kutinga robo fainali ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League].

Denmark walionekana kuuchukua mchezo mapema baada ya kutangulia kwa mabao ya kipindi cha kwanza ya Rasmus Hojlund (Dk. 11) na Pierre-Emile Hojbjerg [Dk. 14], kabla ya ubao kupinduka.

Haaland alifunga bao la kwanza kwa upande wa Norway katika dakika ya 34, Odegaard akapachika jingine dakika ya 83, kabla ya straika huyo wa Manchester City kufunga ukurasa kwa bao la penalti dakika ya 93.

Norway walipata faida ya mkwaju huo wa penalti baada ya teknolojia ya VAR kubaini kuwa beki wa kati wa Denmark, Joachim Andersen, aliunawa mpira ndani ya boksi.

Related articles

Recent articles