LONDON, Uingereza
BAADA ya kukubali ofa ya mkataba mpya, kiungo wa Arsenal, Declan Rice, atakuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo.
Rice, ambaye ana mechi 82 za timu ya Taifa ya England, amekuwa kwenye meza ya mazungumzo ya mkataba mpya kwa muda mrefu.
Nyota huyo alisajiliwa na Arsenal mwaka 2023 akitokea West Ham United, ambapo dili hilo liligharimu kiasi cha Pauni milioni 105.
Mkataba wake wa sasa unaomfanya kulipwa Pauni 250,000 kwa wiki, unatarajiwa kufikia ukomo mwaka 2028 na huu aliongeza utafikia ukomo mwaka 2031.
Kwa mujibu wa ripoti, kwa sasa atakuwa analipwa Pauni 300,000 kwa wiki, hivyo kuwa mchezaji wa bei mbaya zaidi katika klabu hiyo.


