16 C
New York

Zaha mbioni kurudi EPL?

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Crystal Palace iko mbioni kumrejesha Ligi Kuu ya England [EPL] winga wake wa zamani raia wa Ivory Coast, Wilfried Zaha.

Zaha, ambaye alicheza mechi 450 akiwa na Palace, amekuwa akifanya mazoezi na timu hiyo tangu alipoachana na Charlotte FC ya Marekani.

Kabla ya kudumu kwa muda mfupi na Charlotte, nyota huyo aliwahi kuzitumikia Lyon ya Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki baada ya kuondoka Palace.

Palace wako hoi msimu huu kwani wanashika mkia kwenye msimamo wa EPL wakiwa na pointi saba pekee katika mechi 10.

Ifahamike kuwa Zaha ni miongoni mwa wachezaji wenye heshima kubwa katika klabu ya Palace kwani kipaji chake kiliibuliwa na ‘academy’ yao miaka mingi iliyopita.

Related articles

Recent articles