13.9 C
New York

Nchi zinazotegemea zaidi misaada ya Marekani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KWA mwaka 2025, Ukraine ndiyo nchi iliyopokea misaada mingi ya nje kutoka Marekani. Taifa hilo la Ulaya Mashariki lilipokea Dola za Marekani bilioni 6.75.

Katika nafasi ya pili, ni Israel iliyopokea msaada wa Dola bilioni 3.31 kutoka kwa Marekani, ambao ni washirika wakubwa wa kisiasa na kiuchumi.

Jordan inashika nafasi ya tatu kwani kwa mwaka 2025 ilipokea kitita cha Dola bilioni 1.65, huku ‘Top 10’ ikikamilishwa na mataifa ya Afrika.

Ethiopia inaongoza kwa upande wa Afrika, ambapo ilipokea msaada wa Dola milioni 920, ikifuatiwa na DRC [Dola Mil. 750], Nigeria [Dola Mil. 730], na Sudan [Dola Mil. 709].

Aidha, nchi zingine ni Kenya [Dola Mil. 655], Msumbiji [Dola Mil. 584], Uganda [Dola Mil. 513], Sudan ya Kusini [Dola Mil. 507], na Somalia [Dola Mil. 498].

Related articles

Recent articles