LONDON, Uingereza
LIGI Kuu ya England [EPL] imeshuhudia maajabu mengi, likiwamo hili la baadhi ya wachezaji kusifika kwa uwezo wao wa kubadili matokeo kila wanapotokea benchi.
Mathalan, kwa sasa Theo Walcott anabaki kuwa ndiye mchezaji aliyetokea benchi mara
nyingi [168] katika historia ya EPL. Katika michezo hiyo akiwa na Arsenal, Everton na Southampton, bado aliweza kufunga mabao 10 na kutoa ‘asisti’ 14.
Victor Anichebe
Akizitumikia kwa nyakati tofauti klabu za Everton, West Brom na Sunderland, straika huyo aliweza kufunga mabao 13 na asisti tano akitokea benchi.
Kwa ufupi, katika mabao 26 ya EPL aliyofunga nyota huyo raia wa Nigeria, nusu yake [50%] alifunga akiwa ameingia kipindi cha pili.
Daniel Sturridge
Kwa sasa, mshambuliaji huyo ana umri wa miaka 35 na anakipiga Chelsea. Aliwahi pia kupita katika klabu za Manchester City, Bolton, Liverpool na West Brom.
Katika mabao yake 76 aliyowahi kufunga EPL, 17 yalipatikana akiwa anatokea benchi. Wakati huo huo, aliweza kutoa asisti saba.
Olivier Giroud
Katika mabao 90 za EPL akiwa na klabu mbalimbali, ikiwamo Arsenal, Mfaransa huyo aliweza kufunga mara 21 akiwa mchezaji anayetokea benchi.
Kwa misimu 10 aliyocheza Arsenal na Chelsea, Giroud alicheza mechi 103 akiwa anaingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine.
Tore Andre Flo
Flo, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, alifunga mabao 38 ya EPL, huku 12 [34%] akiyapata akiwa mchezaji aliyeingia kipindi cha pili.
Alifunga bao lake la kwanza akitokea benchi katika mechi yake ya kwanza tu akiwa Chelsea mwaka 1997. Kwa ujumla, alitoa asisti tatu katika mechi zake za kutokea
benchi.
Javier Hernandez
Aliwahi kupita Manchester United na baadaye West Ham United. Katika mechi 78 alizotokea benchi, alifunga mabao 19, sawa na asilimia 36.
Kwa takwimu zilivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Mexico alikuwa na wastani wa kufunga bao katika kila dakika 88 alizocheza akiwa anatokea benchi.
Edin Dzeko
Akiwa na umri wa miaka 40 kwa sasa, bado Dzeko anaendelea kufanya vizuri akiwa na Schalke ya Bundesliga.
Dzeko akiwa Manchester City alifunga jumla ya mabao 50 ya EPL, huku 17 na asisti 17 akiwa anatokea benchi. Ni wastani wa bao moja kila baada ya dakika 63 za mchezo.
Ole Gunnar Solskjaer
Akiwa Man United, Solskjaer aliweza kufunga mabao 91 ya EPL, huku 17 yakipatikana akitokea benchi. Moja ya hayo ni lile la kusawazisha wakati Man United ikiifunga Bayern Munich na kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 1999.
Kwa upande mwingine, atakumbukwa kwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 10 wakati Man United ikiondoka na ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Nottingham Forest.
Nwankwo Kanu
Akiwa Arsenal, Mnigeria huyo alicheza mechi 119 za EPL na 56 kati ya hizo ni zile alizoingia akitokea benchi. Alifunga mabao 17 akiwa mchezaji wa kipindi cha pili.
Mbali na kufunga idadi hiyo ya mabao, pia Kanu aliyecheza kwa misimu sita Arsenal, atakumbukwa kwa asisti zake 12 akiwa anatokea benchi.
Jermain Defoe
Ndiye mchezaji anayeongoza kwa mabao mengi ya EPL akiwa anatokea benchi. Alifumania nyavu mara 24. Katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi hiyo akiwa na West Ham United, alifunga mara sita akitokea benchi.
Wakati huo huo, Defoe aliyewahi pia kupita Sunderland, ndiye mchezaji mwenye mabao mengi [7] katika historia ya timu ya Taifa ya England ‘Three Lions’.


