13.9 C
New York

Nchi zinazoongoza kwa kununua ‘drones’ duniani

Published:

Na mwandisi wetu, Gazetini

KUANZIA mwaka 2022 hadi 2025, Ukraine imeagiza ndege zisizo na rubani 8,664. Idadi hiyo ni zaidi ya nusu [51.5%] ya ‘drones’ zote 16,822 zilizoagizwa duniani kote, kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya SIPRI Arms Transfers.

Mpango wa Serikali ya Ukraine ni kufikisha drones 200,000 kwa miaka 10 ijayo, idadi ambayo ni mara 10 ya zilizoagizwa na mataifa yote kuanzia mwaka 2022 hadi 2025.

Maadui zao, Urusi, wanashika nafasi ya pili kwa uagizaji mkubwa wa ndege hizo. Iliagiza 6,720 [39.9%] kuanzia mwaka 2022 hadi 2025. Sehemu kubwa ya drones hizo ni Shahed-136 zilizotoka Iran.

Kwa pamoja, nchi hizo za Ulaya ya Mashariki, Ukraine na Urusi, zimeagiza asilimia 91 ya drones zilizoagizwa duniani kuanzia mwaka 2022 hadi 2025.

Kwa mujibu wa SIPRT, ukiacha Ukraine na Urusi, hakuna nchi nyingine iliyofikisha uagizaji wa walau drones 300 ndani ya miaka mitatu hiyo.

Wakati Ukraine ikiitegemea zaidi Marekani, kwa asilimia 83, Urusi imekuwa ikiagiza sehemu kubwa ya drones zake kutoka Iran, ingawa kwa sasa pia imeongeza uzalishaji wa ndani.

Mbali na Ukraine na Urusi, Taiwan inafuata katika nafasi ya tatu, ambapo imeagiza drones 291 [1.7%], ikifuatiwa na Korea ya Kusini iliyoagiza 190 [1.1%].

Kwa barani Afrika, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo [DRC] ndiyo nchi iliyoongoza kwani imeagiza drones 29, sawa na asilimia 0.2 ya zile zilizogizwa duniani.

Related articles

Recent articles