NEW YORK, Marekani
RAIS wa Marekani, Donald Trump, amekutana ana kwa ana na mwenzake wa Venezuela, Delcy Rodríguez, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Trump kukutana ana kwa ana na Rais huyo wa mpito wa Venezuela tangu Marekani ilipomng’oa Nicolás Maduro.
Trump na Rodríguez wamekutana umbali wa kilometa chache kutoka katika Gereza la New York anakoshikiliwa Maduro akisubiri mashitaka ya dawa za kulevya yanayomkabili.
Katika taarifa yake, Rodríguez amedai kuwa mazungumzo yake na Trump yalilenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Marekani na Venezuela.
Aidha, alienda mbali zaidi na kusema maeneo waliyozungumzia zaidi katika kikao chao ni nishati, madini na usalama.


