LONDON, Uingereza
NI nyota wawili pekee kutoka Afrika walioingia ‘Top 30’ ya kinyang’anyiro cha kuiwania tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or kwa upande wa soka la wanawake.
Nyota hao ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Zambia, Barbra Banda, na mwenzake wa Malawi, Temwa Chawinga.
Banda na Chawinga wameingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kufanya vizuri katika fainali za WAFCON zilizofanyika hivi karibuni, ambapo Cameroon ilitwaa ubingwa.
Chawinga alifunga mabao matano, kama ilivyo kwa Chawinga lakini alimzidi Mmalawi huyo kwa asisti moja.
Je, nani kati yao ataweza kuibeba Afrika kwa kuitwaa tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Mwaka? Ni suala la kusubiri na kuona.


