PRAIA, Cape Verde
KIPA wa timu ya soka ya Taifa ya Cape Verde, Vozinha, ametajwa kwenye orodha ya wanaoiwania tuzo ya mwaka huu ya Ballon d’Or.
Vozinha (40), anawania kipengele cha Kipa Bora baada ya kiwango chake kizuri katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia.
Hata hivyo, anakabiliwa na kibarua kigumu mbele ya Emiliano Martínez wa Argentina, Edouard Mendy wa Senegal, na makipa wengine nane.
Taarifa zinaeleza kuwa mshindi wa tuzo hiyo anatarajiwa kutangazwa Oktoba, 2026, itakayofanyika jijini London, Uingereza.
Makipa wengine walio kwenye kinyang’anyiro hicho ni Yassine Bounou, Thibaut Courtois, Joan García, na Gregor Kobel.
Wengine kwenye orodha hiyo ya makipa Bora 10 ni David Raya, Matvey Safonov na Unai Simon.


