26.8 C
New York

De Jong fiti kuivaa Getafe

Published:

CATALUNYA, Hispania

KOCHA wa Barcelona, Hansi Flick, amefichua kuwa kiungo wake, Frenkie de Jong, atakuwa fiti wiki chache zijazo.

Flick amezungumzia hayo kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi.

De Jong anauguza majeraha ya enka na kwa mujibu wa kocha Flick, ataiwahi mechi yao dhidi ya Getafe itakayochezwa Oktoba 11, 2026.

Awali, Barcelona walikubali afanyiwe upasuaji lakini mchezaji huyo raia wa Uholanzi alikataa na kuchagua tiba ya njia mbadala.

Taarifa zinaeleza kuwa De Jong ameshaanza mazoezi mepesi lakini bado hajaanza kuchezea mpira.

Related articles

Recent articles