19.7 C
New York

Sikia hii ya Bayern, noma sana!

Published:

MUNICH, Ujerumani

KWA mara ya kwanza baada ya mechi 59, Bayern Munich wamelazimishwa kumaliza dakika 90 bila kupata bao.

Ni katika mchezo wa Bundesliga uliochezwa jana Septemba 5, 2026, ambapo Bayern ikiwa ugenini iliambulia suluhu (0-0) mbele ya Schalke.

Bayern waliuanza msimu huu wa 2026-27 kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya VfB Stuttgart, kisha ushindi mwingine mnono wa 4-1 dhidi ya Osnabruck (mchezo wa DFB Pokal).

Katika mchezo dhidi ya Schalke, ni kama Vincent Kompany anaweza kujilaumu kwa uamuzi wake wa kuwaanzishia benchi mastaa wake wawili, Harry Kane na Michael Olise.

Kwa upande mwingine, Kane ambaye ilikuwa mechi yake ya 96 ya Bundesliga, alihitaji mabao mawili tu kufikisha 100 katika mechi zake za Ligi Kuu hiyo.

Related articles

Recent articles