LONDON, Uingereza
KIUNGO mkongwe, Luka Modric, ataendelea kuitumikia timu yake ya Taifa ya Croatia, licha ya umri wake mkubwa wa miaka 41.
Chama cha Soka cha Croatia kimeeleza kuwa nahodha huyo ameonesha nia ya kuendelea na majukumu yake kikosini.
Uamuzi wake wa kutokustaafu unakuja baada ya kocha Slaven Bilic naye kurejea kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.
Bilic aliyewahi kuinoa West Ham, ana mchango mkubwa katika safari yake ya mafanikio akiwa na timu ya Taifa, wakati huo akiwa kocha kati ya mwaka 2006 na 2012.
Katika kipindi hicho, ndipo Modric alipocheza mechi yake ya kwanza akiwa na kikosi hadi kufikisha michezo 202.


