19.7 C
New York

Haaland awafunika Ronaldo, Mbappe

Published:

MANCHESTER, Uingereza

BAADA ya kuifungia Manchester City bao pekee katika mchezo dhidi ya Coventry City, Erling Haaland amefikisha mabao 300 katika maisha yake ya soka la ngazi ya klabu.

Cha kushangaza, Haaland mwenye umri wa miaka 26 ametumia mechi chache (384) kuliko walizokuwa wamecheza Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappe wakati wanafikisha mabao 300.

Ronaldo akiwa na klabu kadhaa, alitimiza idadi hiyo ya mabao akiwa na mechi 499, wakati Mbappe naye alicheza mechi 398.

Hata hivyo, bado Mbappe hajamfikia Lionel Messi, ambaye alifikisha mabao 300 ya ngazi ya klabu akiwa amecheza mechi 365 tu.

Katika historia yake ya klabu, Haaland amezitumikia Molde, Red Bull Salzburg, Borussia Dortmund na sasa Man City.

Related articles

Recent articles