26.2 C
New York

Vigogo wa Marekani waingia Urusi, Ukraine

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

VIGOGO wawili wa serikali ya Marekani, Steve Witkoff na Jared Kushner, wamezitembelea Urusi na Ukraine wikiendi hii.

Ripoti zinaeleza kuwa ziara hiyo imelenga kuleta upatanishi kati ya nchi mbili hizo zilizo kwenye vita kwa miaka minne sasa.

Kwa upande wake, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amethibitisha kuwa atakutana na kufanya mazungumzo na ujumbe huo wa Marekani.

Kabla ya kikao hicho, Witkoff na Kushner watakuwa Urusi leo Septemba 5, 2026, ambapo watakutana na Rais Vladimir Putin.

Witkoff na Kushner wamekuwa wakiongoza timu ya Rais wa Marekani, Donald Trump, inayosaka suluhu kati ya Urusi na Marekani.

Taarifa za wajumbe hao zinakuja zikiwa ni saa chache tangu Zelensky aliposema ndege isiyo na rubani ya Urusi imeishambulia ofisi ya kiongozi wa usalama wa Ukraine, Oleksandr Poklad.

Related articles

Recent articles