21.3 C
New York

Simba kuzima moto, rekodi ya Mighty Wanderers?

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SIMBA iko ugenini mjini Blantyre, Malawi, ambako kesho Septemba 6, 2026, itaumana na Mighty Wanderers katika mchezo wa hatua ya awali msimu huu wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Mighty Wanderers ni mabingwa mara 26 wa mashindano makubwa ya ndani katika soka la Malawi, yakiwamo tisa ya Ligi Kuu na mengine tisa ya Kombe la FA.

Aidha, hautokuwa mchezo rahisi kwa Wekundu wa Msimbazi, ikizingatiwa wenyeji wao wana rekodi ya kutokufungwa katika mechi 10 mfululizo walizocheza hivi karibuni.

Katika michezo hiyo, Mighty Wanderers wameshinda sita na kufungwa minne, wakifunga jumla ya mabao 21 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara tano pekee.

Hata hivyo, bado haimaanishi kuwa Simba haiwezi kupata bao. Katika mechi 10 hizo, ni nne pekee ambazo Mighty Wanderers waliondoka uwanjani wakiwa hawajaruhusu bao [clean sheet].

Kwa sasa, Mighty Wanderers wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Malawi, wakiwa wameshuka dimbani mara 14, wakishinda nane, sare tano na kufungwa mmoja, hivyo kukusanya pointi 29, sawa na Silver Strikers iliyoko kileleni [kwa tofauti ya mabao].

Silver Strikers, ambao pia wana mechi 14, wamefunga mabao 23 na kuruhusu Matano, wakati Mighty Wanderers wao wamepachika 26 lakini nyavu zao zimetikiswa mara tisa.

Wakati huo huo, Mighty Wanderers ni timu isiyo na rekodi nzuri katika mechi zake za nyumbani msimu huu wa Ligi kwani imeshinda mechi tatu pekee kati ya saba, ikifungwa moja na kutoa sare tatu.

Pia, katika mechi saba walizocheza mbele ya mashabiki wao, licha ya kufunga mabao 12, safu yao ya ulinzi nayo imeonekana kutokuwa imara kwani imeruhusu nyavu kutikiswa mara sita.

Related articles

Recent articles