LONDON, Uingereza
DIRISHA kubwa la usajili wa kiangazi Ligi Kuu ya England [EPL] lilifungwa Septemba 1, 2026, huku kiungo aliyetoka Chelsea na kutua Manchester City, Enzo Fernandez, akiandika historia mpya.
Manchester City walitumia Pauni milioni 125 kumng’oa Stamford Bridge na sasa Muargentina huyo anakuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya EPL, akikabana koo na straika wa Liverpool, Alexander Isak, ambaye pia alisajiliwa kwa kiasi kama hicho akitokea Newcastle United.
Mchezaji anayefuata kwa usajili wake kugharimu fedha nyingi ni Morgan Rogers baada ya Chelsea kuipa Aston Villa kiasi cha Pauni milioni 117.
Anayefuata ni Elliot Anderson, ambaye Nottingham Forest imemruhusu kuondoka baada ya Manchester City kulipa ada ya Pauni milioni 116.
Enzo anarudi tena kwa usajili wake kutoka Benfica kwenda Chelsea, ambao uligharimu kitita cha Pauni milioni 106.8.
Bradley Barcola aliyetua Liverpool akitokea PSG naye anaingia kwenye orodha hiyo, ambapo usajili wake umegharimu Pauni milioni 106.
Aidha, Jack Grealish anafuata kwani usajili wake kutoka Aston Villa kwenda Manchester City uligharimu Pauni milioni 100, kiasi ambacjo pia kilitumiwa na Liverpool kumng’oa Florian Wirtz katika klabu ya Bayer Leverkusen.
Nyota mwingine wa bei mbaya katika historia ya EPL ni Declan Rice kwani West Ham United walimwachia kwenda Arsenal baada ya kupewa Pauni milioni 100, kiasi ambacho pia Chelsea waliipa Brighton kumpata Moises Caicedo.


