LAGOS, Nigeria
SUPASTAA wa muziki wa Afrobeats, Davido, amefichua kuwa atastaafu hivi karibuni ili apate muda mwingi wa kutengeneza mabilioni.
Davido amekuja na kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (Twitter).
Aidha, ujumbe wake huo umemlenga rapa Erigga, ambaye hivi karibuni aliwapongeza wanamuziki ‘waliotoboa’ wakitokea familia masikini.
“Hongera kwa wanamuziki wote ambao hawatokei familia zenye pesa na wanaopambania kila Dola wanayoingiza,” alisema Erigga.
Davido, kwa upande wake, amepingana na kauli hiyo, akisema hata wasanii wanaotokea ‘ushuani’ wana uwezo wa kufanya kazi kwa bidii na kupata pesa zao.


