20.9 C
New York

Arsenal, Chelsea vita nzito wikiendi hii

Published:

LONDON, Uingereza

JUMAPILI ya wiki hii, Septemba 5, 2026, Arsenal watakuwa katika Uwanja wao wa Emirates kumenyana na Chelsea kwenye ‘derby’ ya Jiji la London.

Ifahamike kuwa hiyo inakuwa mechi ya tatu kwa kila timu tangu msimu huu wa 2026-27 wa Ligi Kuu ya England.

Washika Bunduki wa London wameshinda mechi mbili zilizopita, wakizifunga Coventry City (3-0) na Aston Villa (1-0).

Kwa upande wao, Blues nao wameshinda michezo yote miwili ya awali, wakitoka kupata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Brighton.

Katika mchezo wao wa kwanza waliokuwa ugenini, walipata pointi tatu kwa kuifunga Fulham ya London mabao 3-2.

Hivyo, wakati Arsenal ikiwa imefunga mabao manne, safu yao ya ulinzi haijaruhusu bao. Chelsea wao wana mabao saba lakini nyavu zao zimetikiswa mara tano.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, atawakosa mabeki wake wawili, Jurrien Timber na William Saliba, ambao wote wanaendelea kuuguza majeraha.

Kwa upande wa Blues, kocha Xabi Alonso atawakosa Jordan Henderson, Marco Palestra na Moises Caicedo wanaoendelea na matibabu.

Kabla ya mechi ya keshokutwa, Arsenal na Chelsea zimeshawahi kukutana mara 215. Washika Bunduki wanaongoza wakiwa na ushindi mara 88, wakati Chelsea imeshinda 66, na sare 61.

Kwa mechi za Ligi Kuu, timu hizo zimekutana mara 67, ambapo Arsenal imeshinda 27, Chelsea imeshinda 20, huku zikipatikana sare 20.

Wakati huo huo, rekodi zinaonesha kuwa Blues wamepoteza mechi zote nne za Ligi walizokwenda Emirates hivi karibuni. Mara ya mwisho kwao kupata ushindi wa Emirates ilikuwa mwaka 2021.

Related articles

Recent articles