BEIJING, China
MATAIFA ya Iran na China yameendeleza uhusiano wao mzuri wa kidiplomasia baada ya viongozi wake wa ngazi za juu serikalini kukutana mjini Bishkek.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ndiye aliyekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa China,
Wang Yi.
Pande mbili hizo zimekutana katika Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Ushirikiano la Shanghai (SCO) mjini Bishkek, kwa mujibu wa taarifa kutoka Tehran.
China, kwa upande wake, imeeleza kuwa bado inalinda mahusiano yake na Iran, licha ya vikwazo vya kiuchumi vilivyotangazwa na Marekani.
Marekani inaendesha kampeni za kuzitaka nchi zote duniani kutokufanya biashara na Iran, pia ikitishia kuzigonga na vikwazo endapo zitakiuka.


