22.3 C
New York

Mahakama: Keffe D ndiye aliyemuua Tupac

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MAHAKAMA nchini Marekani imemkuta na hatia kiongozi wa zamani wa genge la uhalifu, Duane Davis ‘Keffe D’, katika kesi ya mauaji ya rapa Tupac Shakur.

Hatima ya kesi hiyo inafikiwa ikiwa ni miaka takribani 30 tangu Tupac alipouawa kwa kupigwa risasi mwaka 1996 jijini Las Vegas.

Baada ya upelelezi,Mahakama imebaini kuwa Keffe D ndiye aliyempiga risasi Tupac wakiwa kwenye foleni siku hiyo ya Septemba 7, 1996.

Hata baada ya hukumu kusomwa akiwa mahakamani, Keffe D ameweka wazi kuwa wanasheria wake watakata rufaa kuipinga.

Kwa upande wao, ndugu wa Tupac nao walikuwa mahakamani na walionekana wakikumbatiana kuonesha kuridhishwa na hukumu hiyo.

Tupac aliuawa akiwa na umri wa miaka 25, wakati huo akiwa katika kilele cha mafanikio yake kwenye soko la muziki wa Hip hop. Kazi zake zimeuza nakala zaidi ya milioni 75 duniani kote.

Related articles

Recent articles