Na mwandishi wetu, Gazetini
UCHUMI wa dunia unatarajiwa kufikia Dola za Marekani trilioni 150 ifikapo mwaka 2030, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Hata hivyo, nchi tatu za zenye nguvu kubwa ya kiuchumi kwa sasa zinatarajiwa kuwa na utajiri huo huo hata baada ya miaka minne ijayo.
Nchi hizo ni Marekani, ambayo kwa sasa uchumi wake ni Dola bilioni 37.7, China (Dola bilioni 26) na Ujerumani (Dola bilioni 6.2).
Kwa pamoja, nchi hizo zinatarajiwa kuchangia Dola trilioni 10 kwenye uchumi wa dunia ifikapo mwaka 2030.
Kufikia mwaka huo, Marekani pekee itakuwa inachangia asilimia 25.1, ikifuatiwa na China (17.3%), Ujerumani (4.1%), India (4.1%), Uingereza (3.4%) na Japan (3.3%).
Nchi zingine zinazorajiwa kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa dunia ifikapo mwaka 2030 ni Ufaransa (2.7%), Brazil (2.1%), Italia (2.0%), Canada (2.0%), Urusi (1.7%) na Mexico (1.7%).
Wakati huo huo, pia kuna Australia (1.7%), Hispania (1.6%), Korea ya Kusini (1.5%), Indonesia (1.4%), Uturuki (1.3%), Uholanzi (1.1%), Saudi Arabia (1.1%), na Poland (0.9%).


