19.9 C
New York

IRGC: Hormuz haitafunguliwa vitisho dhidi ya Iran vikiendelea

Published:

TEHRAN, Iran

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limetangaza kuwa Mlango Bahari wa Hormuz hautafunguliwa kikamilifu ikiwa vitisho vya kijeshi na kauli za uchokozi kutoka Marekani vitaendelea, likionya kuwa hali ya usalama katika eneo hilo bado ni tete.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Iran (IRNA), IRGC imesema vitisho vinavyoendelea pamoja na kile ilichokiita kuingiliwa kwa harakati za meli katika eneo hilo, vimeongeza mvutano na kufanya mazingira ya usalama kuwa magumu zaidi.

“Vitisho na uingiliaji vimeifanya hali kuwa ngumu na tata zaidi,” imesema IRGC katika taarifa yake.

Jeshi hilo pia limeonya kuwa nchi yoyote itakayoshirikiana na Marekani katika mashambulizi dhidi ya Iran itakabiliwa na hatua kali, ingawa halikutaja nchi yoyote kwa jina.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani Mashariki ya Kati (CENTCOM) kusisitiza kuwa IRGC haina mamlaka ya kuamua njia ambazo meli za kimataifa zinapaswa kutumia katika Mlango Bahari wa Hormuz.

Mlango Bahari wa Hormuz ni mojawapo ya njia muhimu zaidi duniani za usafirishaji wa mafuta na gesi, ambapo sehemu kubwa ya mafuta yanayouzwa kimataifa hupitia katika njia hiyo. Kauli za pande hizo mbili zimeibua wasiwasi kuhusu usalama wa usafirishaji wa nishati na athari zinazoweza kujitokeza katika soko la mafuta duniani ikiwa mvutano utaendelea kuongezeka.

Related articles

Recent articles