23.6 C
New York

Rais Trump ageuka mchambuzi, amvaa Tuchel

Published:

MIAMI, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amekosoa mbinu za kocha Thomas Tuchel akisema ndizo zilizoigharimu timu ya soka ya taifa ya England katika nusu fainali yao dhidi ya Argentina.

Katika mechi hiyo, England walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Anthony Gordon, kabla ya Argentina ya Lionel Messi kusawazisha (Enzo Fernandez) na kufunga jingine (Lautaro Martinez lililowapeleka fainali.

Tangu ulipomalizika mchezo huo, Tuchel raia wa Ujerumani amekuwa kwenye wakati mgumu wa kubebeshwa lawama, licha ya kujitetea kuwa alikuwa sahihi kwa mbinu alizotumia.

Sasa, kwa maoni yake, Rais Trump anaamini Tuchel aliharibu kila kitu alipoanza kujilinda baada ya kuitangulia Argentina kwa bao 1-0.

Akizungumzia matokeo hayo, amesema: “Una wachezaji Harry (Kane). Nafikiri (Tuchel) alifanya kosa kumtumia kama mlinzi.”

Related articles

Recent articles