26.6 C
New York

Huyu Mbappe ni moto mwingine kabisa

Published:

BOSTON, Marekani

MSIMU huu wa fainali za Kombe la Dunia umekuwa wa mafanikio makubwa kwa mshambuliaji wa timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe.

Si tu Ufaransa yake imetinga hatua ya nusu fainali, bali pia ameshafunga mabao nane kati ya 16 ya timu hiyo.

Wakati huo huo, nyota huyo wa Real Madrid ameweka na kuvunja rekodi nyingi tangu fainali za Kombe la Dunia zilipoanza Juni 11, 2026.

Mbappe amefikisha mabao 64 akiwa na Ufaransa, hivyo kumwacha mbali Olivier Giroud anayeshika nafasi ya pili akiwa na 57.

Mkongwe Thierry Henry anashika nafasi ya tatu kwa mabao 51, kisha akifuatiwa na Antoine Griezmann (44).

Katika michuano ya Kombe la Dunia, ndiye mfungaji bora wa timu hiyo kwenye historia ya mashindano hayo. Ana mabao 14, akifuatiwa na Fontaine (13).

Kwa upande mwingine, Mbappe na Lionel Messi ni wachezaji pekee katika historia ya Kombe la Dunia wenye mabao mengi yasiyotokana na penalti. Kila mmoja ana mabao 17.

Mbappe amefikisha mabao 20 tangu alipoanza kucheza Kombe la Dunia, akizidiwa moja tu na nahodha huyo wa Argentina.

Pia, historia ya Kombe la Dunia inamtambua Mbappe kama mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi (12) katika mechi za hatua ya mtoano.

Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na wakongwe wa soka la Brazil, Leonidas na Ronaldo De Lima.

Vilevile, Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza kuchangia (kufunga na asisti) mabao 11 katika misimu miwili tofauti ya Kombe la Dunia.

Aidha, straika huyo anaungana na kipa Hugo Lloris kuwa wachezaji waliocheza mechi nyingi (20) za Kombe la Dunia wakiwa na jezi za Ufaransa.

Related articles

Recent articles