24.9 C
New York

Trump atishia kuishambulia tena Iran leo usiku

Published:

WASHINGRON, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema Marekani inaweza kuanzisha mashambulizi mengine makubwa dhidi ya Iran, akidai kuwa operesheni za kijeshi zilizofanyika usiku uliopita zilikuwa na athari kubwa.

Akizungumza na wanahabari alipokuwa akihudhuria mkutano wa NATO, Trump amesema: “Tuliwashambulia sana jana usiku. Tutawashambulia tena kwa nguvu kubwa usiku wa leo,” amesema.

Trump amedai kuwa mashambulizi yajayo yanaweza kulenga miundombinu muhimu ya Iran, ikiwemo madaraja na kampuni zinazohusika na uzalishaji wa maji safi kupitia uchakataji wa maji ya bahari.

Aidha, amesema Marekani inaweza kuchukua udhibiti wa Kisiwa cha Kharg, kituo kikuu cha Iran cha usafirishaji wa mafuta, akisisitiza kuwa Tehran haina uwezo wa kuzuia hatua hiyo endapo itaamuliwa.

Rais huyo ameongeza kuwa kuna uwezekano wa kutokea “shambulio kubwa” dhidi ya Iran usiku huo, kauli iliyoongeza taharuki kuhusu hali ya usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kauli za Trump zinakuja baada ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, kuonya kuwa mashambulizi yanaweza kufanyika katika maeneo ya ndani kabisa ya Iran, hatua inayozidisha hofu ya kuongezeka kwa mvutano kati ya mataifa hayo.

Related articles

Recent articles