20.5 C
New York

Kibabage aipa mzuka Serengeti Boys kuelekea fainali ya AFCON

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

BEKI wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Nickson Kibabage  amesema kitendo cha vijana wa timu ya Serengeti Boys kufika  fainali ya AFCON – U17 na kiwango walichoonesha ni fursa ya  kwenda kucheza soka la kulipwa katika mataifa makubwa.

Serengeti Boys inatarajia kushuka dimbani kesho  kuchuana na Senegar katika mchezo wa fainali wa michuano hiyo katika Uwanja wa Moulay Hassan, Rabat nchini Morocco.

Kibabage ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji waliunda kikosi cha Serengeti Boys iliyofanya vizuri mwaka 2016,  ametoa kauli hiyo leo  Juni 1, 2026, akiwapongeza vijana hao kwa kuandika historia ya pekee.

Amesema ni jambo la kupongeza kwa sababu Tanzania haijawahi kucheza fainali hizo,  akiamini  Serengeti Boys ina uwezo wa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kutokana na kiwango walichoonesha katika michezo yote.

“Kwanza tunawapongeza kwa hatua walitofikia, ni jambo la kihistoria na kesho wanakwenda  kukamilisha historia. Ni moja jambo kubwa sana kwa nchi yetu Tanzania, haijawahi kutokea hususani kwa timu za vijana kufika hatua hii”, amebainisha.

Related articles

Recent articles