13.5 C
New York

Hapatoshi! Ni nusu fainali ya wanawake Ligi ya Mabingwa Ulaya

Published:

BERLIN, Ujerumani

TIMU ya soka ya wanawake ya Arsenal ndiyo mabingwa watetezi na sasa wataivaa Lyon katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nusu fainali nyingine kali ni ile itakayozikutanisha Barcelona na Bayern Munich.

Katika mechi ya kesho Aprili 26, 2026, Barcelona wanafukuzia kufika fainali ya michuano hiyo kwa mara ya sita mfululizo.

Bayern ndiyo timu pekee iliyopo nusu fainali, ambayo haijawahi kufika hatua ya mwisho (fainali).

Hata hivyo, wametoka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa msimu wa nne mfululizo huko Ujerumani.

Katika mechi ya mwisho kuzikutanisha timu hizo, Barceloina waliibuka na ushindi mnono wa mabao 7-1.

Barcelona wanasaka taji lao la nne la Ligi ya Mabingwa baada ya kufungwa na Arsenal katika fainali ya msimu uliopita.

Arsenal dhidi ya Lyon ni nusu fainali ya keshokutwa Aprili 27. Timu hizo zilikutana nusu fainali ya msimu uliopita na Arsenal ilifanikiwa kusonga mbele.

Lyon ya Ufaransa imefungwa mara moja pekee msimu huu, kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Wolfsburg.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img