9.5 C
New York

Makocha wanaosikilizia kibarua Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

CHELSEA haina kocha mkuu baada ya kumfungashia virago Liam Rosenior, ambaye aliajiriwa Januari, 2026 kuchukua nafasi ya Enzo Maresca.

Rosenior amefutwa kazi akiwa ameiongoza timu hiyo katika mechi 23 pekee. Hatua ya kufukuzwa imekuja baada ya Blues kufungwa mabao 3-0 na Brighton.

Hicho kilikuwa ni kipigo cha tano mfululizo kwa Chelsea kwenye mechi za Ligi Kuu ya England (EPL).

Kwa sasa, Blues inahusishwa na makocha kadhaa barani Ulaya ili kuziba pengo la Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 41.

Andoni Iraola

Mhispania huyo ameshaweka wazi kuwa huu ni msimu wake wa mwisho kwenye benchi la ufundi la Bournemouth. Ameinoa timu hiyo katika mechi zaidi ya 120.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Chelsea wameshaanza mawasiliano na kocha huyo. Iraola ana umri wa miaka 43.

Filipe Luis

Beki wa kushoto wa zamani wa Blues, ambaye alicheza mechi 26 kabla ya kurejea Atletico Madrid.

Amekuwa nje ya kazi ya ukocha tangu alipofukuzwa na Flamengo ya Brazil miezi miwili iliyopita. Inaelezwa kuwa ameshaanza mazungumzo na Chelsea.

Cesc Fabregas

Aliwahi kucheza Arsenal na Chelsea akiwa eneo la kiungo. Ni kocha wa Como ya Serie A na mkataba wake utafikia ukomo Juni, 2028.

Fabregas raia wa Hispania, yuko mbioni kuandika historia ya kuwa kocha wa kwanza kuiwezesha timu hiyo kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Oliver Glasner

Kocha raia wa Austria, ambaye ameshasema ataondoka Crystal Palace mwishoni mwa msimu huu. Amekuwa na timu hiyo tangu Februari, 2024.

Chelsea pia imeripotiwa kufanya mazungumzo na kocha huyo wa zamani wa Eintracht Frankfurt. Anapewa nafasi kubwa ya kuajiriwa Stamford Bridge.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img