LONDON, Uingereza
KATIKA kipindi hiki ambacho Arsenal inapaswa kushinda mechi tano zilizobaki msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL), nyota wake muhimu aliyekuwa majeruhi anakaribia kurejea.
Achana na Bukayo Saka. Taarifa zinaeleza kuwa staa mwingine tegemeo, Mikel Merino, yuko mbioni kupona majeraha yake.
Kiungo huyo raia wa Hispania, amekuwa nje ya uwanja tangu Januari, 2026, alipoumia katika kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Manchester United.
Kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City wikiendi iliyopita kimeongeza presha kwa Arsenal iliyoko kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Kwa sasa, ikiwa imebakiza mechi tano, inaongoza Ligi kwa tofauti ya pointi tatu pekee, ikifuatiwa na Manchester City yenye michezo sita.