6.4 C
New York

Iran: Marekani isijisumbue, vita bado mbichi

Published:

TEHRAN, Iran

MSEMAJI wa jeshi la Iran ametoa kauli ngumu akiimbia Marekani kuwa inapoteza muda katika mpango wa kutaka pande mbili hizo kukaa mezani.

“Watu kama sisi hatutokaa mezani kukubaliana jambo na watu wa aina hiyo (Marekani),” amesema Msemaji huyo.

Kauli yake imekuja baada ya Donald Trump kuonesha utayari wake wa kuzungumza na viongozi wa Iran ili kumaliza vita vinavyoendelea.

Katika taarifa yake ya Machi 24, 2026 kwamba Iran imeipa Marekani kiasi kizuri cha pesa ili kumaliza vita.

Trump alienda mbali zaidi akidai kuwa Marekani imeipa Iran masharti kadha, ikiwamo kuitaka kuacha uzalishaji wa silaha za nyuklia ili kuondoshewa vikwazo ilivyowekewa.

Wakati huo huo, Israel ambao ni washirika wakubwa wa Marekani wameendelea kutupiana makombora na Iran.

Katika mashambulizi hayo, watu sita wameripotiwa kupoteza maisha huko Kusini mwa Lebanon.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img