13.9 C
New York

Visual| Marais ving’ang’anizi wa madaraka duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

FEBRUARI 28, 2026 imeingia kwenye kumbukumbu baada ya kuwa ndiyo siku aliyouawa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika  mashanbulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel yanayoendelea nchini humo.

Kwa upande mwingine, Ali Khamenei ameondoka akiwa mmoja ya viongozi watatu waliokaa madarakani muda mrefu.

Ali Khamenei ameaicha dunia akiwa ameiongoza Iran kwa miaka 36 na miezi sita (Juni 1989 hadi Februari 2026).

Ikumbukwe, alikuwa Rais wa Iran kuazia mwaka 1981 hadi 1989, kabla ya kuwa Kiongozi Mkuu (Supreme Leader) wa Taifa hilo la Kiarabu.

Ikimaaisha, Ali Khamenei amekuwa kwenye ngazi za juu kabisa za uongozi wa Iran kwa miaka takribani 45 mfululizo.

Hata hivyo, Ali Khamenei si kiongozi pekee kati ya walioyaongoza mataifa yao kwa muda mrefu, na badala yake anashika nafasi ya tatu duniani.

Paul Biya (Cameroon)

Miaka takribani 50 akiwa madarakani. Biya alikuwa Waziri Mkuu wa Taifa hilo kuanzia Juni 30, 1975, kabla ya kuwa Rais kuanzia Novemba 6, 1982. Ana umri wa miaka 93.

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo (Guinea ya Ikweta)

Miaka 47 akiwa madarakani. Alikuwa kiongozi wa Baraza la Kijeshi kuanzia Agosti 15, 1979, kabla ya kuingia Ikulu mwaka 1982.

Denis Sassou-Nguesso (Congo Brazzaville)

Ana miaka 42 akiwa madarakani. Kabla ya urais, Sassou-Nguesso aliwahi kuwa Kamanda wa jeshi nchini humo. Alikuwa Rais kuazia mwaka 1979 hadi 1992, kabla ya kurudi mwaka 1997 hadi leo hii.

Yoweri Museveni (Uganda)

Amekuwa Rais wa Taifa hilo la Afrika Mashariki kwa miaka 40 tangu alipoanza kuliongoza mwaka 1986. Museveni, anayefahamika kwa historia ya kutokea familia ya ufungaji, ana umri wa miaka 81.

Emomali Rahmon (Tajikistan)

Amekuwa Rais wa nchi hiyo tangu mwaka 1992. Rahmon amekuwa akikosolewa kwa ushindi wa ‘figisu’ dhidi ya wapinzani katika chaguzi zote alizoshinda nchini humo.

Isaias Afwerki (Eritrea)

Amekuwa Rais wa Taifa hilo kwa miaka 33, tangu alipoingia Ikulu mwaka 1993. Wanaharakati wa haki za binadamu wanadai Eritrea ina wafungwa wa kisiasa zaidi ya 10,000.

Alexander Lukashenko (Belarus)

Kwa miaka 32, Lukashenko amekuwa Rais wa Belarus. Ni tangu alipoingia madarakani mwaka 1994. Ndiye kiongozi aliyedumu muda mrefu zaidi barani Ulaya.

Ismail Omar Guelleh (Djibouti)

Guelleh, maarufu kwa jina la ‘IOG’ (kifupi cha majina yake matatu), amekuwa Rais tangu mwaka 1999, sawa na miaka 27 madarakani.

Vladimir Putin (Urusi)

Miaka 27 akiwa Rais wa Urusi. Baada ya kushika nafasi nyingi za uongozi tangu mwaka 1999, Putin alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais mwaka 2000. Alimaliza mwaka 2008, kisha akareja mwaka 2012 hadi leo hii.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img