15.6 C
New York

CAF yaisogeza mbele WAFCON

Published:

CAIRO, Misri

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza kuzisogeza mbele fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake (WAFCON).

Awali, michuano hiyo ilitarajiwa kuanza Marchi 17, 2026, lakini sasa ni Julai 25 hadi Agosti 16, 2026.

“Baada ya mazungumzo kati yetu na wadau, FIFA na wadau wengine, CAF tumeamua kupanga WAFCON ifanyike kuanzia Julai 25-Agosti 16, 2026 ili kuhakikisha inafanikiwa zaidi,” imeeleza taarifa ya CAF.

Hata hivyo, CAF haikueleza kwa kina sababu iliyopelekea mashindano hayo yasifanyike kama ilivyopangwa awali (Marchi 17, 2026).

Wakati huo huo, taarifa hiyo inakuja zikiwa ni wiki takribani tatu tu tangu Rais wa CAF, Patrice Motsepe, aliposema hakuna mabadiliko yoyote yatakayofanyika katika ratiba ya WAFCON.

Kwa upande mwingine, zipo taarifa kwa wiki kadhaa sasa, kwamba Morocco inaweza kujitoa katika uenyeji wa fainali hizo.

Aidha, Serikali ya Afrika Kusini imeweka wazi kuwa Iko tayari kupokea kijiti endapo Morocco itajitoa kuandaa michuano hiyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img