LONDON, Uingereza
KLABU za Manchester United na Chelsea zimeripotiwa kukanusha ripoti zinazodai kuwa zimewasiliana na kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp.
Klopp, raia wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 58, amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Anfield mwishoni mwa msimu wa 2023-24.
Wakala wake, Marc Kosicke, amesisitiza mara kadhaa kuwa upo uwezekano wa kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund kurejea katika benchi la ufundi.
Pia, ni Kosice ndiye aliyewahi kufichua kuwa mabosi wa Man United na Chelsea wamefanya mazungumzo na mteja wake huyo.
Mbali ya Man United na Chelsea, klabu ya Real Madrid nayo imekuwa ikitajwa kumuweka kwenye rada zake kocha huyo.


