18.1 C
New York

Mastaa hawa wanajutia kuzihama timu zao

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

UMESHAWAHI kusikia msemo wa ‘usajili ni kamari’? Kwamba wakati mwingine mchezaji anayefanya vizuri akiwa na klabu moja anaweza ‘kupotea’ baada ya kuhamia kwingine.

Mifano ni mingi lakini makala haya yanaangazia wale waliopotea katika maamuzi ya kuzihama klabu zao wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka 2025.

James Trafford

Akiwa kipa wa daraja la juu, aliondoka Burnley na kujiunga na matajiri wa jijini Manchester, Manchester City.

Trafford aliahidiwa angekuwa chaguo la kwanza langoni lakini ujio wa Gianluigi Donnarumma umefuta nafasi yake kikosini.

Tetesi za usajili zinadai kuwa tayari mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 23 anaangalia uwezekano wa kukimbia Etihad mwishoni mwa msimu huu.

Trent Alexander-Arnold

Alikuwa mmoja ya mabeki wa kulia bora kabisa kuwahi kutokea Ligi Kuu ya England (EPL), wakati huo akiwa na Liverpool.

Usajili wake wa kujiunga na Real Madrid umemtoa kwenye reli kwani hapati namba mbele ya Dani Carvajal na zipo taarifa zinazodai kuwa anajutia uhamisho huo.

Kwa kukosa nafasi, nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anajiweka hatarini kutokuitwa katika kikosi cha England kitakachoshiriki Kombe la Dunia mwaka huu.

Darwin Nunez

Mshambuliaji huyo aliondoka Liverpool na kutua Al-Hilal ya Saudi Arabia. Kwa sasa, inaelezwa kuwa hana furaha klabuni hapo.

Mambo yamekuwa mabaya zaidi kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 baada ya Al-Hilal kumsajili straika wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema.

Hivi karibuni, wakati wa usajili wa dirisha dogo la Januari, 2026, Nunez alikaribia kutua Fenerbahce lakini dili liliota mbawa dakika za mwisho.

Liam Delap

Mshambuliaji huyo alikuwa tishio kwa upachikaji mabao akiwa na Ipswich Town lakini sasa mambo ni magumu pale Chelsea.

Si tu imekuwa ni ngumu kwake kupata nafasi ya kucheza, bali pia Delap amefunga bao moja tu kwenye Ligi msimu huu.

Mkongwe wa Liverpool, Jamie Carragher, anaamini Chelsea ni timu kubwa kwa mchezaji aliyetoka chini kama Delap. “Kutoka Ipswich hadi Chelsea ilikuwa ni hatua kubwa, alihitaji kwanza kucheza timu za madaraja ya kati,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img