18.1 C
New York

CAF yaipa Kenya siku 90 tu

Published:

NAIROBI, Kenya

TIMU ya wakaguzi ya Shirikisho la Soka l Afrika (CAF) haijaridhishwa na kiwango cha maandalizi yaliyofanyika kwa ajili ya fainali zijazo za AFCON zitakazofanyika hapo mwakani.

Ni kwa maana hiyo, CAF imeipa Kenya siku 90 kuhakikisha inakamilisha baadhi ya miradi, ikiwamo miundombinu ya viwanja vitakavyotumika.

Kenya kwa kushirikiana na majirani zao wa Afrika Mashariki, Uganda na Tanzania, zitaandaa michuano hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, viwanja vikubwa vya Kasarani na Nyayo pia havijawavutia maofisa wa CAF walipofika kwa ajili ya ukaguzi.

Maeneo yaliyotajwa kuwa na kasoro ni pamoja na taratibu za usalama, mfumo wa kudhibiti mashabiki na hata ubora wa sehemu ya kucheza (pitch).

Kile kilichoelezwa na maofisa hao ni kwamba maandalizi yanapaswa kukamilika miezi sita kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.

Ikumbukwe, michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni, 2027, hivyo maandalizi yakamilike Desemba 26, 2026.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img