MERSEYSIDE, England
BABA mzazi wa Alexis Mac Allister, Carlos, amesema kiungo huyo wa Liverpool kwa sasa haifikirii klabu yoyote zaidi ya ‘Majogoo’ hao wa Anfield.
Carlos, ambaye pia ndiye wakala wa Mac Allister, amesema hayo, licha ya kwamba Manchester United inajaribu kumsajili nyota huyo mwishoni mwa msimu huu.
Mbali ya Mac Allister, Man United pia inatajwa kuwaweka kwenye rada zake viungo wengine watatu; Carlos Baleba, Adam Wharton na Elliot Anderson.
“Akili ya Alexis iko Liverpool tu kwa sasa. Tunasubiri ofa ya kuongeza mkataba mpya. Ngoja tuone mipango ya klabu,” amesema Carlos.
Kwa sasa, nyota huyo raia wa England anawania namba na viungo watatu pale Anfield, ambao ni Ryan Gravenberch, Dominik Szoboszlai na Curtis Jones.
Mac Allister amefunga mabao 17 na kutoa ‘asisti’ 17 katika mechi 132 alizocheza tangu alipotua Anfield mwaka 2023. Mkataba wake utakwisha mwaka 2028.


