LONDON, Uingereza
NI miezi miwili pekee tangu mwaka 2026 ulipoanza na tayari kuna orodha ya mastaa wa soka waliotangaza kuachana na mchezo huo.
Je, ni akina nani hao? Makala haya yanakuibulia wachezaji watatu waliotangaza kutundika daluga mwaka huu.
Marco van Ginkel
Nyota huyo wa zamani wa Chelsea, AC Milan, Stoke City na timu ya taifa ya Uholanzi amestaafu akiwa na umri wa miaka 33 tu.
Kwa muda mwingi, alicheza kwao akiwa na PSV na Vitesse. Mechi zaidi ya 100 akitumikia klabu hizo.
Miralem Pjanic
Kiungo wa zamani wa Roma, Juventus na Barcelona. Raia huyo wa Bosnia alibeba mataji saba akiwa Juve, moja akiwa Barca, pia tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka akiwa Roma.
Katika timu ya taifa ya Bosnia, alistaafu akiwa amecheza mechi zaidi ya 100. Huyo ndiye Pjanic, ambaye pia alipita Lyon.
Mamadou Sakho
Aliwahi kupita Liverpool akitokea PSG. Alipokuwa na vigogo hao wa Ligue 1 alibeba makombe saba.
Maisha yake akiwa Liverpool hayakuwa mazuri. Msimu wake wa kwanza walishika nafasi ya pili (msimamo Ligi Kuu). Alistaafu akiwa Torpedo Kutaisi ya Ligi Kuu nchini Georgia.


