NAIROBI, Kenya
VIGOGO wa Ligi Kuu ya Kenya, Sofapaka FC, wamefanya balaa zito kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo, ambapo imetema wachezaji 11.
Mkakati huo ni katika ‘kujitafuta’ chini ya kocha mpya, Abdalla Juma, ambaye ameikuta timu hiyo ikiwa kwenye hali mbaya msimu huu.
Sofapaka, ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya mwaka 2009, wamekusanya pointi 14 pekee, licha ya kushuka dimbani mara 19.
Katika usajili wao, mabosi wa Sofapaka wametupa macho nchi za Rwanda, Albania, Ghana, Nigeria, Congo, huku pia wakizibomoa baadi ya klabu za Kenya.
Je, usajili huo utaiimarisha Sofapaka na kuipa taji la Ligi Kuu lililopotea klabuni hapo kwa miaka takribani 17?


