18 C
New York

Kozi ngumu, zenye mishahara mikubwa

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

“UVUMILIVU ni mchungu lakini matunda yake ni matamu.” Ni msemo unaotafsiri maisha mazuri wanayoishi waajiriwa baada ya mateso ya ‘kozi’ ngumu walizosomea wakiwa vyuo vikuu nchini Marekani.
Baadhi ya kozi ziliwachukua miaka sita, nane hadi 10 kuweza kuhitimu. Je, ni kozi zipi hizo zinazolipa vizuri, licha ya ugumu wake darasani?

Unajimu

Ugumu wa kozi hii ni kwamba inahusisha hisabati, fizikia na kemia katika kujifunza kuhusu vitu kama nyota na sayari. Kwa Marekani, mwanafunzi hutumia hadi miaka 10 akiwa chuo kikuu, ingawa mshahara wake ni mzuri kwani muhitimu aliyeajiriwa huwa na uhakika wa mshahara wa hadi Dola 149,530 kwa mwezi.

Udaktari

Kama ilivyo duniani kote, kozi ya udaktari ni ngumu na si wanafunzi wengi wanaoichukua wanapoingia vyuo vikuu. Kwa Marekani, huchukua hata miaka nane kwa mwanafunzi kuhitimu.

Nchini humo, mwanafunzi atasoma kwa miaka mitatu hadi saba lakini atahitaji tena mwaka mmoja wa darasani ili kupata leseni ya kufanya kazi katika jimbo fulani. Mshahara ni takribani Dola 239,200.

Uhandisi wa Ndege

Itachukua miaka sita kwa mwanafunzi kusomea kozi hii nchini Marekani. Ni taaluma inayohusisha hesabu kwa kiasi kikubwa na inajikita katika ubunifu, upimaji na usimamizi wa utengenezaji wa ndege.

Licha ya ugumu na muda wingi anaotumia mwanafunzi akiwa chuo kikuu, atakuwa na uhakika wa kulipwa mshahara unaofikia Dola 130,720 kwa mwezi nchini Marekani.

Udaktari wa meno

Kwa Marekani, itamchukua mwanafunzi miaka mitano kuweza kuhitimu, kisha mwaka mmoja au miwili kupata leseni. Lakini, habari njema ni mwamba ataingia kwenye soko la ajira akiwa na uhakika wa mshahara usiopungua Dola 170,910 kwa mwezi.

Uhandisi wa mitambo

Kwa Marekani, ni miaka mitatu tu ya kuhitimu Shahada ya kwanza, kisha kuingia kwenye soko la ajira lenye ofa ya mshahara wa Dola 99,510 kwa mwezi.

Hata hivyo, wahitimu wengi wa kozi hii hupenda kuendelea kwa walau mwaka mmoja au miwili ili kupata Shahada ya Uzamili (master’s degree).

Sheria

Ni kozi ngumu kwa wanafunzi wengi. Inahitaji muda mwingi kujisomea. Ni wachache wanaoichagua, ingawa ni kozi inayowavutia wengi kutokana na hadhi yake mbele ya jamii. Kwa Marekani, miaka mitatu tu inatosha kwa muhitimu kupata Shahada yake ya kwanza, ingawa atahitaji mwaka mwingine mmoja wa Shule ya Sheria (Law School). Mshahara si chini ya Dola 145,760 kwa mwezi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img