10.6 C
New York

Maumivu makali sekta ya afya nchini Iran

Published:

TEHRAN, Iran

MADUKA mengi ya dawa yamefungwa, imekua ngumu hata kwa akina mama kujifungulia hospitalini, huku uhaba wa dawa na vifaa tiba nao ukiendelea kuiumiza sekta ya afya nchini Iran tangu kuanza kwa vita vyake na Marekani.

Mitra, mkazi wa Tehran mwenye umri wa miaka 37, ni mmoja ya wagongwa wa kisukari wanaopitia wakati mgumu kipindi hiki kutokana na uhaba wa dawa zake.

“Dawa zangu si zile unazoweza kusema utaacha kuzitumia. Maisha yangu yanategemea kuzipata kila baada ya muda mfupi,” amesema.

Taarifa zinataja sababu ya hali mbaya hiyo kuwa ni kuporomoka kwa thamani ya fedha ya Iran, hivyo viwanda vya ndani vinavyotengeneza dawa kufilisika.

Pia, hospitali nyingi, zikiwamo za Serikali, zimetajwa kushindwa kulipa madeni kwa wasambazaji wa dawa hizo, hivyo kusitishiwa huduma.

Wiki chache zilizopita, Iran iliripotiwa kukosa dwa muhimu takribani 40 kati ya 700 hazipatikana sokoni kwa sasa kwenye sekta ya afya nchini humo.

Mmoja ya wamiliki wa duka la madawa mjini Tehran ameeeleza kuwa malipo ya bima kwa wagonjwa wanaowahudumia yamekuwa yakichelelewa kwa miezi kadhaa, wakati huo bei ya dawa ikiwa imepanda.

Hivyo, maduka ya madawa yameshindwa kuhimili mtikisiko huo, ikizingatiwa kuwa wasambazaji wamekuwa wakihitaji kulipwa fedha taslimu ili kutoa huduma.

Si tu Tehran, hali ni mbaya pia mjini Mahabad, ambako duka kubwa la madawa linaweza kukosa hadi dawa muhimu zaidi ya 100, zikiwamo zile za magonjwa mazito, kikiwamo kisukari.

Kutokana na hali hiyo, umeibuka utamaduni mbaya wa uuzaji wa dawa kinyemela, tena kwa bei isiyofuata utaratibu.

Hivyo, wanaomudu kuzipata kutokana na bei zake, ni wananchi wenye kipato kikubwa, huku wazee, watoto na wanawake wa Maisha ya kawaida wakielezwa kutaabika zaidi.

Hayo yote yanatokea huku viongozi wa Iran na Marekani wakiendelea kutunishia misuli, kila upande ukigoma kuonesha nia ya dhati ya kumaliza vita.

Related articles

Recent articles